Majaliwa azindua matumizi ya nishati safi ya kupikia kwenye magereza

0

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Agosti 30, 2025 amemwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika uzinduzi wa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia katika Magereza 129 nchini.

Uzinduzi huo umefanyika katika gereza la Karanga lililopo Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa niaba ya magereza yote nchini.

Mpaka sasa vyanzo vya nishati mbadala vinayotumika katika magereza ni Gesi Vunde (BIOGAS), Mkaa Mbadala (Briquettes), Kuni Poa na Gesi Asilia (NATURAL GAS) na umeme.

Majaliwa alisema, hatua hiyo ni ya kupongeza kwa kuwa inaunga mkono maono ya Rais Dkt. Samia ya kuhakikisha jamii yote inatumia nishati hiyo na hivyo kwa kiasi kikubwa kuondoa madhara yatokanayo na matumizi ya nishati isiyo safi.

Akizungumza wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu, Msimamizi wa Kitengo cha Kilimo, Mifugo na Utunzaji wa Mazingira kutoka Jeshi la Magereza SACP Daimu Mmolosha amesema lengo la jeshi hilo ni kuhakikisha kunakuwa na chanzo zaidi ya kimoja cha nishati ili kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here