NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali (OWM- TAMISEMI), Reuben Kwagilwa amesema, Serikali inatarajia kujenga mtandao wa barabara za lami zenye urefu wa Kilometa 257 katika mkoa wa Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP II unaolenga kuboresha miundombinu yote ya msingi zikiwemo barabara.
Naibu Waziri Mhe. Kwagilwa ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Nchi, OWM- TAMISEMI, Prof. Riziki Shemdoe, wakati akijibu swali la Nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Kawe Geofrey Timoth, aliyetaka kujua ni lini Serikali itazifanyia ukarabati barabara kadha zinazopita kwenye jimbo lake la kawe kuelekea maeneo mengine ya mkoa wa Dar es Salaam.
Amefafanua kuwa kupitia mradi wa DMDP II Serikali imetenga Dola
Milioni 438 za Kimarekani ambazo ni sawa na Shilingi Tirioni 1 na Bilioni 131 za Kitanzania, kwa ajili ya kuendeleza miundombinu yote ya msingi zikiwemo barabara za mkoa mzima wa Dar es Salaam.