JAMII imeaswa kujiepusha na matumizi ya WI-FI za bure (Free wifi) ili kulinda taarifa zao binafsi.
Ushauri huo umetolewa hivi karibuni Mkoani Morogoro na Mkuu wa Uhusiano na Mawasiliano PDPC, Innocent Mungy wakati akitoa mada ya Wajibu wa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kwenye Mafunzo Maalumu ya Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi ambapo alisema, ili kulinda taarifa zako binafsi jihadhari na mitandao ya bure.
“Duniani hakuna kitu cha bure, mimi nimeacha kutumia free WiFi baada ya kugundua baadhi ya watu wanatumia mbinu hiyo kudukua taarifa zangu binafsi kupitia kifaa cha kieletroniki ninachotumia iwe simu janja, kompyuta mpakato au tablet”
Aidha, katika hatua nyingine Mungy amewatoa wito kwa Maafisa Ulinzi wa Taarifa Binafsi kuhakikisha wanaweka ombi la ridhaa kwenye ofisi zao kama wanatumia CCTV kamera.
“Ombi la Ridhaa lipo kisheria kupitia Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi Sura ya 44 hivyo kama ofisini yako inatumia CCTV kamera nakushauri uweke Ombi hilo ili kila anaeingia aridhie kuchukuliwa kwa taarifa zake ikiwemo picha mtembeo (video).