Dugange: Uhakika wa matibabu kwa wahanga Hanang ni 100%

0

Na Mwandishi Wetu

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange amewahakikishia majeruhi wa maafa ya maafuriko wanaotibiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini pamoja na vituo vingine vya kutolea huduma wilayani Hanang kuwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba upo kwa asilimia 100 na hakuna mgonjwa yeyote atatozwa fedha kwa ajili ya matibabu.

Dkt. Dugange ameyasema hayo alipotembelea hospitali hiyo kuangalia hali za majeruhi sambamba na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba.

“Niwahakikishie kama ambavyo imeelekezwa na Rais wetu Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan majeruhi wote wa maafa haya wanapata matibabu bila kulipia gharama zozote.”

“Nitoe Rai kwa watoa huduma wetu wa afya kutekeleza kwa weledi maelekezo ya Serikali kwa kuwahudumia wajeruhi wa mafuriko usiku na mchana bila kuchoka ili waweze kupata nafuu na kurejea kwenye majukumu yao ya kila siku,” alisema Dkt. Dugange.

Katika hatua nyingine, Dkt. Dugange alikuwa miongoni mwa viongozi walioambatana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwajulia hali manusura wa maafa ya mafuriko waliotengewa eneo katika Shule ya Sekondari Katesh.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here