Dkt. Mwinyi: Z’bar inaendelea kuweka mazingira bora ya uwekezaji

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar inaendelea Kuweka Mazingira Mazuri zaidi ya Kuwavutia Wawekezaji zaidi Kuwekeza nchini .

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza na Balozi wa Tanzania nchini Nigeria, Balozi Selestine Gervas Kakele aliefika Ikulu Zanzibar Januari 14, 2025.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa kuna fursa kubwa ya Nchi hizo mbili kushirikiana hasa katika Sekta ya Utalii na Uwekezaji ambazo zikifanyika vyema nchi hizo zinaweza kunufaika kwa kiasi kikubwa.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amemsisitiza Balozi Kakele kufanya juhudi Maalum za kuwavutia Wawekezaji kutoka Nigeria kuja Nchini kuangalia Fursa za Uwekezaji na Serikali inaanda Mazingira mazuri ya kuwa na Uwekezaji wenye tija na Endelevu.

Amefahamisha kuwa Utalii na Uwekezaji ni Vichocheo Muhimu vya Uchumi wa Zanzibar hivyo ni vema akaweka Mkazo katika kuwavutia Wawekezaji katika Maeneo hayo.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa bidhaa nyingi kutoka Afrika Magharibi zinauzwa nje ya Afrika kuliko zile zinazouzwa katika Ukanda wa Afrika kutokana na Kukosekana kwa Kiunganishi cha Ushirikiano wa Kibiashara.

Naye, Balozi Kakele alisema Nigeria ni nchi kubwa na ina fursa nyingi ambazo Tanzania ikiwemo Zanzibar zinaweza kushirikiana hususani Uwekezaji katika Biashara na Huduma za Kibenki na Kushauri kuandaliwa Mazingira Wezeshi ya upatikanaji Viza baina ya nchi hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here