Dkt.Mwinyi: Madhehebu ya dini ni nguzo ya amani

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema madhehebu ya dini yana mchango mkubwa katika kudumisha amani na utulivu wa Taifa.

Akihutubia Kongamano la Kuiombea Nchi Amani lililoandaliwa na Umoja wa Akina Mama wa Kikristo na Maendeleo Zanzibar, Tunguu,Mkoa wa Kusini Unguja.

Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amesema amani ni neema inayopaswa kuenziwa na kila mmoja, huku akisisitiza wajibu wa viongozi wa dini kuwaelimisha waumini kuhusu umuhimu wa amani.

Halikadhalika, amewahakikishia akina mama wa Kikristo kuwa Serikali itaendelea kushughulikia changamoto za taasisi za dini ili ziweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here