Chama kimejipanga kwa ushindi – Wasira

0

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amezungumza na wanachana na viongozi wa Chama wilayani ileje mkoani Songwe akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.

Akizungumza na wana CCM hao katika Ukumbi wa Seselembe, Ileje leo, Machi 16, 2025, Wasira alisema Chama kinaingia katika uchaguzi mkuu wa mwaka kikiwa hakina wawasi wa kushinda kutokana na kazi nzuri iliyofanywa na serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Chama Cha Mapinduzi kinaingia katika uchaguzi kikiwa na hakika ya ushindi kutokana na kazi kubwa ya kuleta maendeleo iliyofanywa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, tunavisihi vyama viingie vya siasa viingie katika uchaguzi huu na wananchi endeleeni kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura,” alisema Wasira.

Awali, baada ya kuwasili wilayani humo akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake kwa Mkoa wa Songwe, Wasira alipokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na hali ya siasa ya wilaya hiyo, kisha kuweka jiwe la msingi ujenzi wa jengo la kitegauchumi cha Chama wilaya ya Ileje na kuongoza uchangiaji wa ujenzi wa jengo hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here