SERIKALI imepanga kutumia shilingi bilioni 1.06 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa la uvuvi na mialo yake katika eneo la Mchinga lililopo Wilayani Lindi ili kudhibiti upotevu wa mazao ya uvuvi na kuongeza thamani mazao hao na kuwanufaisha wavuvi.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dkt. Bashiru Ally Novemba 15, 2026 katika mkutano wa hadhara wakati za Ziara ya Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi Wilayani Lindi, baada ya Mbuge wa Mchinga Salma Kikwete kutaka majibu ya serikali kuwa ni lini soko hilo litaanza kujengwa.
Waziri Balozi Dkt. Bashiru amesema ujenzi wa soko hilo utaendana na uwekaji wa miundombinu yake ya kuhifadhi samaki litajegwa na utekelezaji wake utaanza ndani ya mwaka huu wa fedha 2026/2027 na kwamba tayari serikali imeshatenga fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.06 kwa ajili ya ujenzi wa Soko la Mchinga.
Katika hatua nyingine Balozi Dkt. Bashiru amesema Wizara ya Mifugo na Uvuvi, inaendelea na utafiti kwa ajili ya ufugaji wa samaki wa maji baridi na chumvi katika ukanda wa pwani, ambapo amesema utafiti huo unaendelea kufanyika na hivi karibuni utakamilika.