RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amewatembelea wagonjwa na kuwafariji katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mjini Lumumba, tarehe 1 Aprili 2025.
Wagonjwa waliotembelewa Arafa Mohamed Said na Kanali Mstaafu Mzee Masoud Khamis Juma.
Rais Dkt.Mwinyi amewatakia heri na kuwaombea kupona haraka.
Rais Dkt.Mwinyi amekuwa na utaratibu wa kuwafariji wagonjwa.