Mapokezi makubwa yanamsubiri Dkt. Mwinyi Pemba

0

Mwandishi Wetu, Pemba

MAPOKEZI makubwa yanamsubiri mgombea mteule wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) 2025, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, 15 FebruarI 2025 na kuhutubia wananchi kwenye viwanja vya Kiwani.

Mkutano Mkuu wa dharula wa CCM uliofanyika, Dodoma Jauari 18 na 19 mwaka 2025, kwa kauli moja ulimpitisha na Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu 2025.

Pia, mkutano huo ulimpitisha Steven Wassira kuwa Makamu wa Rais CCM Bara kujaza nafasi ya Abdrahman Kinana na toka Rais Dkt. Mwinyi, achaguliwe na mkutano mkuu CCM Dodoma hivi karibuni, alikuwa hajafika Pemba kutokana na ratiba za shughuli hiyo kuingiliana na uandikishaji daftari la kudumu la wapiga kura, Pemba.

Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis alisema kuwa, awali Dkt. Mwinyi ilikuwa aende Pemba baada ya kupokewa Unguja.

“Uandikishaji wa daftari la wapiga kura, tunamaliza kesho (leo Ijumaa), hivyo kesho Jumamosi atatua Uwanja wa Ndege, Pemba kunako saa tatu asubuhi ambako atakuwa na mkutano wa ndani na wazee wa kisiwa hicho, kabla ya kuelekea viwanja vya Kiwani atakapo hutubia mkutano wa hadhara.” alisema Mbeto.

Mbeto anawataka wananchi kujitokeza kwa wingi kumlaki kisha kuelekea viwanja hivyo na maandamano makubwa ya Bajaj, Bodaboda, magari, baiskeri na kulingana na Mwenezi huyo, Rais Dkt. Mwinyi ana ujumbe mahsusi kuhusiana miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Zanzibar hivi sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here