REA yagawa majiko banifu 200 Mkoani Tanga

0

MWENYEKITI wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ambaye amembatana na Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Wabia wa Maendeleo wamegawa majiko banifu 205 yanayotumia kuni na mkaa kidogo kwa Wanafunzi na Wananchi wa kijiji cha Madumu kilichopo Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga.

Tukio hilo lilifanyika Aprili 4, 2024 katika Shule ya Sekondari Chekelei wakati wa ziara ya Wabia wa Maendeleo iliyolenga kukagua utekelezaji wa Miradi ya kusambaza nishati vijijini.

Katika mwaka huu wa fedha wa 2024/2025; REA imepanga kusambaza majiko banifu 200,000 katika mikoa tofauti ya Tanzania Bara.

Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa wakati akifungua Kongamano la Nishati ya Kupikia jijini Dar es Salaam, Novemba 2022 ambapo lengo la Serikali kupitia REA ni kuhamasisha matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika maeneo yao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here