RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo tarehe 7 Agosti 2026, amefungua rasmi miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT) Awamu ya Pili katika barabara za Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa jijini Dar es Salaam.
Katika hafla hiyo, Rais Dkt. Samia ameambatana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah, jambo linaloakisi ushirikiano wa maendeleo kati ya Tanzania na AfDB katika kuimarisha miundombinu ya usafiri nchini.
Mradi huo unatarajiwa kuboresha huduma za usafiri wa umma, kupunguza msongamano wa magari, kufupisha muda wa safari, na kuongeza ufanisi wa shughuli za kiuchumi pamoja na kuboresha maisha ya wakazi wa Dar es Salaam.