MGOMBEA wa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 amewataka Vijana wa Maswa mkoani Simiyu kujiandaa kutumia vema ujio wa fursa zinazotokana na ujio wa Reli ya Kisasa ya SGR.
Ujenzi huo utaenda sambamba na Kituo cha kushusha na kupakia abiria na mizigo, huku akibainisha kuwa miundombinu hiyo itakuja na fursa za ajira na uchumi kwa wananchi wa Maswa na Simiyu kwa ujumla wake.
Dkt. Samia amesisitiza kuwa moja kati ya dhamira yake na maelekezo ya kitabu cha ilani ya CCM (2025/30) ni kuhakikisha Serikali yake inaendelea kuwainua Vijana kiuchumi kwa kuibua ajira mpya nyingi dhidi yao na kuendelea kuwajengea uwezo wa wao wenyewe kujiajiri.
Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi wa Maswa mkoani Simiyu, Dkt. Samia amesema kamwe CCM haitaacha kuwajali Vijana ndiyo maana imekuwa ikiwagusa katika miradi mbalimbali kama vile Mradi wa Jenga Kesho Bora (BBT), unaosimamiwa na Wizara ya Kilimo ambao umewezesha Vijana zaidi ya 3,000,000 kujiajiri kupitia kilimo.
Akizungumzia sekta ya miundombinu, Dkt. Samia ameahidi kuendelea kuziunganisha wilaya zote zilizopo ndani ya mkoa wa Simiyu kwa barabara za lami na makao makuu ya mkoa pamoja na Barabara kuu za Kata zinazoelekea kwenye makao makuu ya wilaya za mkoa huo wa Kanda ya Ziwa.
Vilevile, amesema Serikali inaendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuondoa changamoto ya wanyamapori vamizi ambao wamekuwa wakitoka katika maeneo yao ya hifadhi na kuvamia wananchi pamoja na mashamba yao ya kilimo.
Katika hilo, Dkt. Samia ameahidi kuendelea kujenga vituo vya askari wanyamapori kwaajili ya kudhibiti wanyama hao pamoja na ununuzi wa vifaa mbalimbali vya ufuatiliaji ikiwemo ununuzi wa ndege nyuki kwaajili ya utambuzi na ufuatiliaji wa wanyama wanaotoka kwenye maeneo yao.
𝙄𝙡𝙞 𝙠𝙪𝙥𝙖𝙩𝙖 𝙢𝙖𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙤 𝙚𝙣𝙙𝙚𝙡𝙚𝙫𝙪, 𝙨𝙝𝙞𝙧𝙞𝙠𝙞 𝙪𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙯𝙞 𝙊𝙠𝙩𝙤𝙗𝙖 29 𝙣𝙖 𝙈𝙘𝙝𝙖𝙜𝙪𝙚 𝘿𝙠𝙩. 𝙎𝘼𝙈𝙄𝘼 𝙠𝙬𝙖 𝙢𝙞𝙩𝙖𝙣𝙤 𝙩𝙚𝙣𝙖 𝙋𝙖𝙢𝙤𝙟𝙖 𝙣𝙖 𝙒𝙖𝙗𝙪𝙣𝙜𝙚 𝙣𝙖 𝙈𝙖𝙙𝙞𝙬𝙖𝙣𝙞 𝙬𝙖 𝘾𝘾𝙈.