MGOMBEA wa Urais wa Zanzibar kupitia CCM, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ijayo itaongeza bajeti na kuwekeza zaidi katika kilimo na ufugaji ili wananchi wanufaike kiuchumi.
✅ Wakulima watapatiwa pembejeo, mbegu bora, mbolea na masoko ya bidhaa zao kwa wakati.
✅ Wafugaji watawezeshwa mikopo isiyo na riba na kuunganishwa na masoko ya uhakika.
✅ Mikopo midogo itawasaidia wananchi kuendeleza shughuli zao za uzalishaji.

Dkt. Mwinyi ameyasema hayo katika mkutano wa kampeni uliofanyika Uwanja wa Michezo Uzini, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja Septemba 16, 2025.
Akihitimisha, amewataka wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ifikapo Oktoba 29, ili kuendelea kuleta maendeleo kwa Zanzibar.
