Kishindo cha Samia sasa ni Zanzibar

0

Na Albert Kawogo

MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewasili Kisiwani Zanzibar leo Septemba 15, 2025 kuanza kampeni pamoja na kumwaga sera.

Dkt. Samia ameingia Zanzibar baada ya kukamilisha kampeni zilizokuwa na mafanikio makubwa mkoani Kigoma.

Alihitimisha kampeni zake huku akiwataka wananchi wa mkoa huo kumpa kura za kishindo pamoja na kuendelea kushirikiana na serikali katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Baadhi ya Miradi mikubwa ambayo amesema itaufungua mkoa wa Kigoma ni pamoja na ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR, maboresho ya bandari na barabara pamoja na usafiri wa anga ambavyo vitaufanya mkoa huo kuwa kitovu cha biashara na uchumi.

Dkt. Samia baada ya kuwasili Zanzibar, alilakiwa na viongozi wa CCM pamoja na wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Ndege wa Abeid Amani Karume.

Mikutano ya kampeni za CCM kisiwani Zanzibar inaanza Septemba 17, ambapo Dkt. Samia atakuwa na kazi ya kuinadi ilani ya chama chake na kuomba ridhaa ya wananchi wa visiwani humo kuendeleza kasi ya maendeleo ya taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here