Uchumi wa Buluu yatajwa kuwa sekta kubwa na muhimu

0

UCHUMI wa buluu umetajwa kuwa ni sekta kubwa na muhimu ambayo kama ikitumika vizuri itaweza kukuza uchumi wa taifa kupitia shughuli mbalimbali nchini.

Akifunga Kongamano la Uchumi wa Buluu jijini Dar es Salaam leo Septemba 11, 2025, Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Prof. Godius Kahyarara amesema sekta hiyo inachagizwa shughuli za uvuvi, nishati na usafirishaji.

Amesema kuwa Serikali ina dhamira ya dhati katika kuendeleza uchumi wa buluu kupitia uwekezaji mkubwa unaofanywa kwenye sekta ya uchukuzi, hususan upande wa bahari na bandari.

Prof. Kahyarara alibainisha kuwa Serikali imeendelea kuboresha miundombinu ya usafiri wa majini ikiwemo ununuzi wa gati mpya kwa ajili ya wavuvi kuhakikisha maazimio ya kongamano hili yanatekelezwa kwa vitendo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI) Prof. Tumaini Gurumo alisema maadhimisho haya yameweka msisitizo kwa wadau kuandaa mipango ya sera na matumizi sahihi ya rasilimali za bahari kwa maendeleo endelevu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here