Tanzania, Burundi zazindua ujenzi wa reli ya SGR Uvinza – Musongati

0

๐Ÿ“Œ Kugharimu Dola za Marekani Bilioni 2.154

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo (Jumamosi, Agosti 16, 2025) ameshiriki uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa ya kutoka Uvinza hadi Musongati na kuwahahikishia Watanzania na WanaBurundi kwamba ujenzi huo utaanza katika muda uliopangwa.

Waziri Mkuu ambaye ameshiriki hafla hiyo kwa niaba ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema reli hiyo itakayokuwa na urefu wa KM 240 pindi ikikamilika, itakuwa ndiyo reli ya kwanza inayounganisha nchi na nchi katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika eneo la Musongati, Burundi, Waziri Mkuu alisema kukamilika kwa ujenzi wa reli hiyo kutasaidia kuunganisha masoko na kuendeleza biashara baina ya Tanzania na Burundi.

โ€œReli ikikamilika itafungua fursa kwa wananchi wetu ambao wataweza kutoka hapa hadi Dar es Salaam ndani ya siku moja. Hata kwenye usafirishaji wa mizigo, hivi sasa, lori linatumia saa 96 kutoka Dar hadi Bujumbura lakini baada ya kukamilisha ujenzi, usafirishaji wa mizigo kwa kutumia treni utatumia saa 20 tu.โ€

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here