MGOMBEA nafasi ya Ubunge wa jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, amewaasa wanachama viongozi ambao ni wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo kuwa makini katika kuchagua na haswa wakijua kuwa ushindi wa Chama Cha Mapinduzi unawategemea wao, hivyo wachague vizuri.
Maneno hayo ameyasema wakati akizungumza na wajumbe hao katika kata ya Ubena, Msoga, Lugoba na Msata.
Katika mkutano huo ambao pia ulilenga kuwatambulisha wagombea nafasi za udiwani, ulitumika kuwakumbusha viongozi hao juu ya majukumu makubwa waliyonayo ya kutangaza mazuri yaliyokwishafanywa katika miaka mitano ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mgombea Kikwete alitumia hadhira hiyo kuwakumbusha mafanikio waliyokwisha yapata katika Sekta mbalimbali ikiwemo miundoMbinu ya Barabara, Afya, Elimu, Maji, uwezeshaji wananchi, maendeleo ya Jamii na kadhalika.
Vikao hivi vinahitimishwa kwa kufanyika kwa zoezi la kupiga kura za maoni kuchagua Madiwani na kumthibitisha Mgombea Ubunge wa jimbo hilo ambaye amepita bila kupingwa Agosti 14, 2025.