Dkt. Mwinyi: Amani ni nyenzo muhimu ya ustawi wa kila sekta

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema kuwa amani ni nyenzo muhimu ya ustawi wa kila sekta katika nchi, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuilinda na kuidumisha, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo Julai 25, 2025 jijini Dodoma, mara baada ya kushiriki Sala ya Ijumaa pamoja na waumini wa dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Ijumaa wa Sunni Muslim Jamaat

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi alisema, viongozi wa dini, wanahabari na wanasiasa ni miongoni mwa watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii, hivyo ni muhimu wakawa mstari wa mbele katika kueneza ujumbe wa amani na mshikamano.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi ameongeza kuwa mifano ya athari za migogoro na machafuko inajionesha wazi kupitia mitandao ya kijamii kutoka mataifa yasiyo na amani.

Kwa upande mwingine, Rais Dkt.Mwinyi ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha kuwa amani inadumishwa kabla, wakati na baada ya uchaguzi kwa ajili ya mustakabali wa Taifa na vizazi vijavyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here