‘Kuweni wabunifu katika kuandaa miradi ya maendeleo’

0

Na Asila Twaha, OR – TAMISEMI

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Adolf Ndunguru amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi, sehemu ya Mipango na Uratibu Makatibu Tawala Wasaidizi Uchumi na Uzalishaji, Maafisa Mipango na Uratibu wa Halmashauri na Waweka Hazina wa Halmashauri kuhakikisha wanakuwa wanakuwa wabunifu.

Lengo ni kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na miradi ya maendeleo itakayoandaliwa na kutekelezwa kwa kuzingatia miongozo na ushauri wa kitaalamu.

Ndunguru ameyasema hayo Juni 13, 2025 jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo kwa wataalamu hao yalikuwa yamefanyika kwa awamu mbili ampapo awamu ya kwanza yamefanyika kuanzia tarehe 3-6 Juni, 2025 na awamu pili yalianza tarehe 10-13 Juni, 2025.

“Serikali ina imani kubwa sana nanyinyi tekelezeni majukumu yenu kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kazi na muwe wepesi wa kueleza mapema changamoto kama zinatokea ili zishughulikiwe kwa wakati” alisema Ndunguru.

Amewataka kwa waweka hazina wanatumia mifumo ya ndani kutunza namba za siri za kuingilia kwenye mfumo wa mapato, kufuatilia fedha zilizokusanywa na hazijawasilishwa benki kwa wakati, kufanya usuluhishi wa kibenki kwa akaunti zote za halmashauri na vituo vya kutolea huduma kwa wakati, matumizi ya TAUSI App (Toleo la Kiganjani) kuhakiki uhalali wa stakabadhi, vibali na leseni na kudhibiti ugawaji wa Float kwa wahasibu wa mapato na wakusanya ushuru.

Ndunguru alisema, dhamira ya Serikali ya kuanzisha na kutekeleza miradi kwa njia ya Special Purpose Vehicle (SPV) na Public-Private Partnership (PPP) ni kuhakikisha inafanikiwa na Ofisi ya Rais -TAMISEMI itaendelea kutoa elimu kwa viongozi wa mikoa, wilaya na halmashauri kwa kuwashirikisha viongozi wa kisiasa ili kuhakikisha wanaelewa vyema malengo ya miradi hiyo ili kuondoa mwingiliano wa majukumu na hivyo kuwezesha utekelezaji wake kwa ufanisi katika ma

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here