Na Subira Ally
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Watanzania wanaoishi na kufanya kazi nchini Oman maarufu Diaspora.
Katika mkutano huo Dkt. Mwinyi aliwaeleza wana Diaspora hao lengo la ziara yake nchini Oman, kwanza ni kuimarisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania Zanzibar hasa na Oman na pia kutafuta fursa za biashara zitakazojenga uchumi.
Aliwafahamisha hali ya utulivu ilivyo Zanzibar na kuwataka kuwekeza kwani ni wakati mzuri sasa kufanya hivyo.
Pia, aliwapo somo kuhusu sera ya uchumi wa buluu na akainisha mambo matano Serikali inavyojikita katika kuingia katika sera hiyo.
Aliyataja mambo hayo kuwa ni Utalii, uimarishaji bandari kubwa kwa ujenzi wa Bandari kubwa eneo la Mangapwani, uchimbaji wa mafuta na gesi na kubainisha , na usafiri wa baharini.
Rais Dkt. Mwinyi alisema yote hayo yaende vizuri ni lazima kuwe na umeme wa uhakika, maji, barabara nzuri na mfumo mzuri wa IT.
Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi pia aliwashukuru wana Diaspora wanaojitolea kwa misaada mbalimbali ya kijamii.
Dk Hussein Ali Mwinyi na ujumbe wake watamaliza ziara ya Oman kesho ijumaa.