WANANCHI wameendelea kutembelea banda la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika eneo la Chinangali Park Dodoma, ambapo wanapata fursa ya kujifunza kuhusu utekelezaji wa miradi ya mawasiliano inayosimamiwa na UCSAF pamoja na mchango wake katika kuboresha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.
Tunawakaribisha wananchi wote kuendelea kutembelea banda la UCSAF ili kujionea mafanikio ya miradi inayotekelezwa, kupata elimu kuhusu juhudi za Serikali katika kupeleka huduma za mawasiliano maeneo mbalimbali nchini, na kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wetu kwa ufafanuzi na maswali mbalimbali.
Karibu banda la UCSAF ujifunze, upate taarifa sahihi na ufahamu zaidi kuhusu nafasi ya mawasiliano katika kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa.