Wahandisi Washauri wanaoshindwa kusimamia wakandarasi wasipewe kazi – Bashungwa

0

WAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kutowapatia kazi za usimamizi wa miradi Wahandisi Washauri wanaoshindwa kuwasimamia Wakandarasi kutekeleza miradi ya ujenzi wa barabara kwa viwango na mujibu wa mikataba na kupelekea Mkandarasi kurudishwa eneo la mradi kurudia kazi.

Bashungwa alitoa maagizo hayo Wilayani Mafia wakati akikagua barabara ya Kilindoni – Utende (KM 14.6) iliyojengwa na Mkandarasi CHICO, chini ya usimamizi wa Mhandisi Mshauri Kampuni ya UWP Tanzania, ambapo barabara hiyo haikutekelezwa kwa viwango na kusababisha Mkandarasi kurudia sehemu ya kazi.

“Kama mlivyofanya katika mradi huu kwa kumrudisha Mkandarasi Site, Wahandisi Washauri kama hawa wanaoshindwa kumsisimamia Mkandarasi wanapaswa wawe ‘blacklisted’ kwa sababu tunawalipa pesa ya kumsimamia Mkandarasi kwa niaba ya Serikali”, alisema Bashungwa.

Bashungwa amemuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kutompatia kazi yoyote ya kusimamia miradi Mhandisi Mshauri wa kampuni ya UWP Tanzania na wahandisi washauri wengine wa aina hiyo ambao wameshindwa kutekeleza wajibu wao kwakuwasimamia Makandarasi kutekeleza miradi kikamilifu na kuisababishia hasara Serikali.

“Mhandisi Mshauri UWP hafai na nikiona mmempa kazi sehemu yotote mimi na nyinyi na hii iwe funzo kwa Wahandisi Washauri wengine tunaowapa kazi ya kuwasimamia Makandarasi”, alisema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa alisema Wizara ya Ujenzi itaendelea kuwasimamia Wakandarasi na Wahandisi Washauri walipatiwa kazi za kutekeleza miradi ili fedha zinazotolewa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ziweze kutekeleza na kukamilisha miradi kikamilifu kama ilivyokusudiwa.

Naye, Kaimu Mkurugenzi wa Miradi kutoka TANROADS Eng. Malima Kusesa ameeleza kuwa, ujenzi wa barabara ya Kilindoni – Utende (KM 14.6) kwa kiwango cha lami ulikamilika mwaka 2015 na baada ya muda wa matazamio 2016 yalibainika mapungufu katika kipande cha Kilometa nne.

Eng. Kusesa ameeleza kuwa baada ya kubainika mapungufu hayo, TANROADS walimtaka Mkandarasi CHICO na Mhandisi Mshauri UWP Tanzania kurudia kazi sehemu hiyo kwa gharama zao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here