TCB wapongezwa kwa kutengeneza faida

0

WAZIRI wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya Benki hiyo na mchango wake katika maendeleo ya Taifa.

Mkutano huo umefanyika Ofisini kwa Waziri wa Fedha Treasury Square, jijini Dodomaambapo Waziri wa Fedha ameipongeza Benki hiyo kwa mafanikio inayoendelea kuyapata ikiwemo kutengeneza faida katika biashara ya sekta ya fedha.

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya Benki hiyo na mchango wake katika maendeleo ya Taifa, Ofisini kwa Waziri wa Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (kulia) akiagana na Mkurugenzi wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, baada ya kumalizika kwa mkutano wao ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya Benki hiyo na mchango wake katika maendeleo ya Taifa, uliofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akieleza umuhimu wa Benki ya TCB katika maendeleo ya Taifa wakati alipokutana na Mkurugenzi wa Benki ya TCB, Adam Mihayo (hayupo pichani), Ofisini kwake, Wizara ya Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Jenifa Christian Omolo, akitoa maelekezo kwa Benki ya TCB ya namna ya kuendelea kuboresha huduma wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba na Mkurugenzi wa Benki ya TCB, Adam Mihayo (hayupo pichani), katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, akielezea umuhimu wa Benki hiyo katika kuchochea ukuaji wa Uchumi, wakati wa mkutano kati yake na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (hayupo pichani), ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya Benki hiyo na mchango wake katika maendeleo ya Taifa, uliofanyika katika Ofisi ya Waziri wa Fedha Treasury Square, jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba, akiongoza mkutano kati yake na Mkurugenzi wa Benki ya TCB, Adam Mihayo, ambapo walijadili kuhusu maendeleo ya Benki hiyo na mchango wake katika maendeleo ya Taifa, uliofanyika Wizara ya Fedha, jijini Dodoma. (Picha Kitengo cha Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Fedha).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here