TARURA Kilombero yajipanga kutekeleza miradi

0
Mhandisi Sadick Karume (Kulia) akikagua moja ya barabara inayosimamiwa na TARURA Wilaya ya Kilombero.

Na Mwandishi Wetu, Kilombero

MENEJA wa TARURA Wilaya ya Kilombero Mhandisi Sadick Karume, amesema wamejipanga vizuri kutekeleza miradi mbalimbali ya barabara ikiwemo inayolalamikiwa na wananchi wa Wilaya hiyo.

Mhandishi Karume alisema, anafahamu changamoto nyingi za barabara zilizopo katika Wilaya hiyo, na wanafanya jitihada kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi.

“Nimesikia baadhi ya malalamiko, niko tayari kuyafanyia kazi na wakandarasi nimewaelekeza kilichobaki ni utekelezaji kwani wananchi wanahitaji huduma bora,” alisema Mhandisi Karume na kuongeza kuwa, wananchi wa Kilombero wanatakiwa kuiamini TARURA kwani wanajitahidi kutekeleza kwa haraka miradi husika.

Karume ametoa wito kwe wakandarasi wote waliopewa kazi katika Wilaya yake kufanyakazi kama walivyokubaliana katika mikataba na TARURA Kilombero imekuwa ikifanya ukaguzi wa mara kwa mara kuona kazi za ujenzi wa barabara inavyoendelea.

Aidha, Mhandishi huyo amewataka wananchi wanaotumia barabara za Namawala kuelekea Mofu kutokuwa na wasiwasi kwani TARURA imesikia kilio chao huku akiwasihi wanaotumia vyombo vya moto katika barabara ambazo bado zipo katika ujenzi kuepuka kuwapa wakati mgumu wakandarasi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here