SERIKALI imetoa fedha kiasi cha Shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Mwamapalala iliyopo katika Kata ya Mwamapalala Wilaya ya Itilima Mkoa wa Simiyu.
Hayo yamebainishwa leo Machi 8,2026 na Muuguzi Mfawidhi wa Zahanati ya Nkololo, Bahati Clavery mbele ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenani Kihongosi alipotembelea mradi huo, ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi katika mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Muuguzi huyo Mfawidhi amesema, mradi huo umetumia zaidi ya Shilingi Milioni 252, ambapo Shilingi Milioni 250 zimetoka Serikali Kuu ambayo hadi sasa imetumika Shilingi Milioni 214 na zilizobaki ni Shilingi Milioni 35, ili kukamilisha mradi. Wananchi wa kijiji cha Mwamapalala wamechangia Shilingi 2,370,000
Akizungumza baada ya kukukagua mrafi huo Kenani Kihongosi alisema ujenzi wa mradi huo unaridhisha huku akimpongeza mkandarasi kwa kazi aliyoifanya kwani inaendana na thamani ya fedha iliyotolewa na Serikali.