Na Cletus Sanga, WAF – Dar es Salaam
SERIKALI imeanza utekelezaji wa hatua mpya za kuimarisha huduma za afya ya uzazi salama nchini, ikilenga kupunguza vifo vya mama na mtoto kupitia maboresho ya huduma za kliniki na huduma za dharura wakati wa kujifungua.
Hatua hiyo imetangazwa Aprili 17, 2026 jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Programu ya Uzazi Salama, Dkt. Phineas Sospeter, wakati wa kikao kazi cha wataalamu wa afya ya uzazi salama.
Amesema maboresho hayo yanajumuisha kuimarisha huduma za kliniki kwa wajawazito, mifumo ya ufuatiliaji wa vifo vya mama na watoto wachanga pamoja na kuongeza uwezo wa watoa huduma kukabiliana na dharura za uzazi.
Aidha, serikali inaendelea kuboresha mifumo ya takwimu za afya ili kusaidia maamuzi sahihi ya kisera na kuhakikisha huduma zinawafikia wananchi kwa ufanisi.