Serikali kumrejesha ‘site’ mkandarasi stendi ya Moshi mjini

0

SERIKALI imeanza mazungumzo na mkandarasi wa Ujenzi wa Stendi ya Ngangamfuni iliyopo Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro ili arejee katika eneo la ujenzi baada ya mkandarasi kuondoka na kusitisha ujenzi kwa kipindi cha miaka miwili.

Kauli ya Serikali imetolewa bungeni na Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI Festo Dugange kwa niaba ya Waziri wan chi Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mohamed Mchengerwa wakati akijibu swali la Priscus Tarimo, mbunge wa Jimbo la Moshi mjini aliyetaka kujua kuwa serikali iko tayari kuvunja mkataba wa ujenzi wa stendi hiyo endapo atakataa kurejea na kuendelea na ujenzi

Akijibu swali hilo Dugange alisema: “kulikuwa na changamoto ya menejimenti ya mkataba kati ya mkandarasi na Halmashauri na kutokana na sababu hizo na tumefanya vikao mwezi Januari na mwezi februari kati ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Halmashauri ya Manispaa ya Moshi na mkoa wa Kilimanjaro kukubaliana na mkandarasi arejee kwenye site aendelee kufanyakazi”

Akisisitiza hilo Dugange alisema, mpaka sasa Serikali imefikia hatua za mwisho za makubaliano na mkandarasi na ikitokea akikataa kuendelea na ujenzi serikali itachukua hatua nyingine ikiwemo kuvunja mkataba kwa mujibu wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here