‘Serikali imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana’

0

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Ridhiwani Kikwete amesema Serikali imejidhatiti kuweka mazingira yanayowezesha vijana kutoka kwenye uchumi usio rasmi kuelekea uchumi ulio rasmi.

“Serikali inaendelea kuimarisha sera zinazowezesha nguvu kazi ya taifa, kuondoa vikwazo vya Kibiurokrasi, kutoa msaada wa kiufundi na kifedha kwa Vijana” alisema.

Ridhiwani amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa uchambuzi wa kina wa sekta isiyo rasmi katika biashara zinazoongozwa na Vijana.

Aidha, alisema tafiti zilizofanywa sekta zisizo rasmi zitasaidia kupata majawabu ya matatizo ya Vijana katika kukabiliana na changamoto isiyo rasmi.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirikia la Kazi Duniani Kanda ya Afrika Mashariki Caroline Mugalla, Mkurugenzi Mtendaji na Afisa Mtendaji Mkuu wa ATE Suzanne Ndomba na Watafiti Mashuhuri.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here