LICHA ya kuifunga Argentina bao 1-0 katika fainali ya Kombe la Dunia 2026, Uhispania haitaruhusiwa kuondoka na kombe halisi la dhahabu.
Uhispania ilitwaa ubingwa wa Kombe la Dunia la FIFA 2026 kwa bao pekee ambalo lilifungwa na Ferran Torres.
Kanuni za FIFA zinaelekeza timu inayoshinda hukabidhiwa kombe wakati wa sherehe za uwanjani mara tu baada ya filimbi ya mwisho, kisha timu hiyo inatakiwa kulirejesha kombe hilo kwa FIFA katika chumba cha kubadilishia nguo kabla ya kuondoka uwanjani.
Badala ya kombe halisi, Uhispania itapokea kile ambacho FIFA inakiita Kombe la Washindi wa Kombe la Dunia la FIFA (FIFA World Cup Winner’s Trophy), ambalo ni nakala ya kombe na chama cha soka cha nchi iliyoshinda kinaruhusiwa kulihifadhi milele kama kumbukumbu ya ushindi wake.
Kombe halisi la FIFA lililotengenezwa kwa dhahabu ya karati 18 na lenye urefu wa sentimita 36, halijawahi kuwa mali ya Taifa lolote lililoshinda tangu muundo wa sasa ulipoanzishwa mwaka 1974.
FIFA ilianzisha sera ya Kombe la washindi mahsusi ili kulinda kombe halisi, huku ikiwapa mabingwa alama ya kudumu ya mafanikio yao.
Kombe la awali, lilikabidhiwa rasmi Brazil mwaka 1970 baada ya Taifa hilo kwa mara ya tatu.