Rais Samia awataka wananchi Kakonko kutunza Miundombinu

0

Na Angela Msimbira, KIGOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kuhakikisha wanatunza miundombinu ya afya inayojengwa na Serikali ili idumu kwa muda mrefu.

Rais Samia alisema hayo leo Oktoba 16, 2022 alipokuwa akizimdua Hospitali ya Wilaya ya Kakonko, Halmashauri ya Wilaya ya Kankoko, mkoani Kigoma iliyojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 2.9.

“Wito wangu kwenu ni kutunza mali yenu, hii si mali ya Serikali, jitahidini kutunza hospitali yenu iwahudumie leo, kesho na kesho kutwa,” alisisitiza Rais Samia.

Alisema, Serikali itaendelea kununua vifaa tiba vya vipimo vyote vinavyohitajika kwa binadamu pale anapotakiwa kuhudumiwa.

Rais Samia alisema, vifaa tiba vimenunuliwa lakini bado vingine havipo, hivyo Serikali itahakikisha inaleta vifaa kwa ajili ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here