Rais Samia amkabidhi nyumba Mama Janeth Magufuli

0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi mfano wa ufunguo mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli ikiwa ni ishara ya kukabidhi nyumba mpya ya kuishi kwa familia ya Dkt. John Pombe Magufuli iliyopo wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam ambayo amejengewa na Serikali kwa mujibu wa sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa nyumba mpya ya Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, na kuikabidhi kwa Mama Janeth Magufuli, nyumba hiyo imejengwa na Serikali kwa mujibu wa sheria, Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mjane wa Hayati Dkt. John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Mama Janeth Magufuli wakati wa hafla fupi ya kukabidhi nyumba ya kuishi iliyopo wilaya ya Kinondoni  Jijini Dar es Salaam.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here