RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amepokea bendera ya Jukwaa la Sera za Utalii kwa Visiwa (ITOP), ikiwa ni ishara rasmi ya Zanzibar kuwa mwenyeji wa Jukwaa la 28 la ITOP mwaka 2027.
Rais Dkt. Mwinyi amekabidhiwa bendera hiyo na Gavana wa Jeju, Mhe. Wi Seong-gon, Oktoba 29,2026, wakati wa hafla ya ufunguzi wa Jukwaa la 27 la ITOP iliyofanyika Jeju Stone Park, Kisiwa cha Jeju, Jamhuri ya Korea (Korea Kusini).
Uenyeji huo utaipa Zanzibar fursa ya kutangaza vivutio vyake vya utalii, utamaduni na uwekezaji, pamoja na kuimarisha ushirikiano na maeneo ya visiwa duniani katika kukuza utalii endelevu na maendeleo ya uchumi.
ITOP ina maeneo 12 wanachama ambayo ni Jeju, Bali, Hainan, Okinawa, Southern Province ya Sri Lanka, Hawai‘i, Zanzibar, Phuket, Cebu, Penang, Galápagos na South Aegean.