Rais Mwinyi amuaga Balozi mdogo wa China

0

RAIS Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi mdogo wa China Zhang Zhisheng anayefanyia kazi zake Zanzibar, kumuaga baada ya kumaliza muda wake wa utumishi nchini.

Rais Dkt. Mwinyi amemshukuru Balozi Zhang Zhisheng kwa kudumisha na kuimarisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Zanzibar na China katika miaka mitatu ya utumishi wake nchini, pia kwa kuratibu vema ziara yake mwaka jana China.

Vilevile, Rais Dkt.Mwinyi ameeleza kuwa China imeendelea kusaidia Zanzibar na kushirikiana katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya kwa kuleta madaktari kutoka China, ufadhili wa masomo, kujengea uwezo, biashara, utalii, pamoja na kuwepo kwa kampuni za kichina katika kazi za miradi mbalimbali ya miundombinu ya barabara, bandari, na uwanja wa ndege.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi amewakaribisha wawekezaji kutoka China kwenye sekta ya utalii kujenga hoteli kwa kuongeza watalii zaidi wa Kichina kuitembelea Zanzibar.

Alisema, Zanzibar itaendelea kushirikiana na kudumisha uhusiano na China ambayo yametimiza miaka 60.

Naye Balozi Zhang Zhisheng alisema, China itaendelea kushirikiana na Zanzibar kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here