RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema Mafanikio ya Ukuaji wa Uchumi wa Tanzania unatokana na usimamizi mzuri wa Uchumi unaofanywa na Benki kuu ya Tanzania (BoT).
Rais Dkt. Mwinyi amesema hayo alipojumuika katika Futari ya Pamoja ilioandaliwa na Benki hiyo katika Hoteli ya Madinat Al Bahr, Mkoa wa Mjini Magharibi Machi 25, 2025.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi alisema amekuwa akifarijika na Ushauri wa Kifedha anaoupata kutoka Benki Kuu katika kusimamia Uchumi wa Zanzibar.
Amebainisha kuwa Mafanikio Makubwa yanayopatikana hivi sasa kwa Uchumi wa Tanzania ikiwemo Zanzibar yamechangiwa na Uimara wa Usimamizi Bora wa Kifedha unaotekelezwa na BoT.
Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi ameipongeza BoT kwa Kuendeleza Utaratibu wa Kuwakutanisha pamoja Wadau wa Benki hiyo kila Mwaka wakati wa Mwezi wa Ramadhani.
Naye Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Emmanuel Mpawe Tutuba amemuhakikishia Rais Dkt. Mwinyi kuwa Uchumi wa Tanzania Uko Vizuri na unaendelea kukua na Sekta ya Fedha inafanya Vizuri na Mfumuko wa bei upo Mdogo .
Amefahamisha kuwa Uchumi wa Tanzania Bara umekuwa kwa Asilimia 5.4 na Zanzibar umekuwa kwa Asilimia 7.