Posta, Simba wajadiliana kuhusu uzinduzi wa ‘Simba Day’

0

MENEJA wa Habari na Mawasiliano kutoka Klabu ya Simba ambaye pia ni Msemaji wa Timu ya hiyo Ahmed Ally ametembelea Shirika la Posta Tanzania na kupokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo Ferdinand Kabyemela Agosti 27, 2025 jijini Dar es Salaam.

Lengo la ziara hiyo ni kufanya mazungumzo kuhusu maandalizi ya tukio la Simba Day ambapo Shirika la Posta ni mmoja wa wadhamini wakuu katika tukio hilo.

Tamasha hilo linategemea kufanyika Septemba 10, 2025 katika Uwanja wa Taifa na Shirika la Posta linategemea kutangaza huduma zake mahsusi za Swifpack na Duka Mtandao la Kipepeo.

Vilevile, Mazungumzo hayo yalihusu uuzaji wa jezi za timu ya Simba ambazo zitaanza kuuzwa mara baada ya uzinduzi huo unaotarajia kufanyika tarehe 31/08/2025 katika ukumbi wa Superdome Masaki na Shirika la Posta ndio litahusika katika uuzaji na usambazaji wa Jezi hizo ndani na nje ya Nchi kupitia Duka Mtandao la Posta linaloitwa Kipepeo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here