Njia za kupata wataalam
Wazalendo zatajwa

0

Na Subira Ally

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Ali Abdulgulam Hussein amesema, Awamu ya Nane imedhamiria kuona sekta ya Elimu inaendelea kupiga hatua kwa kuendelea kupunguza changamoto mbalimbali.

Alisema hayo wakati akifungua kongamano la kitaaluma la siku moja katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar SUZA Kampasi ya Maruhubi Mkoa wa Mjini Unguja.

Alisema, Serikali inaendelea kuboresha miundo mbinu ya kielimu na pamoja na maslahi ya walimu ili Elimu ipatikane Katika mazingira mazuri na salama.

Alisema, historia inaonesha Elimu hapo awali ilipatikana kwa matabaka, lakini baada ya Mapinduzi Elimu ni haki ya lazima kwa kila mtu kuipata.

Hivyo, ameeleza kuwa ili wananchi waitumie haki ya kupata Elimu ni vyema kuimarisha miundo mbinu yote ya kielimu ili kufikia malengo ya Taifa ya kuzalisha wataalam wazalendo kupitia fani mbalimbali.

Nae Mkurugenzi Idara ya michezo Wizara ya Elimu Zanzibar Ahmed Abdallah Mussa alisema, uwepo wa kongamano la kitaaluma ni kuhakikisha jamii inapata kujua historia ya Elimu ilivyoanzia na kuona jinsi inavyoendelea kwa kuhakikisha kila mwananchi anapata haki yake ya kuelimika.

Nao washiriki wa kongamano hilo wamesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imejitahidi kupunguza baadhi ya changamoto, lakini bado wameiomba Wizara ya Elimu kuajiri watu wa ushauri Nasaha kwa kila Skuli kwani Wanafunzi wengi wanaonekana kukosa uwezo wa kufanya vizuri kutokana na msongo wa mawazo.

Kongamano hilo la kitaaluma ni miongoni mwa shamra shamra za kuelekea kilele Cha miaka 58 ya tamasha la Elimu bila ya malipo ambapo huadhumishwa kila mwaka ifikapo Septemba 23.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here