MNEC Asas kufanya ziara maalum Iringa

0
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (MNEC) Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas

Na Andrew Chale

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM (MNEC) Mkoa wa Iringa Salim Abri Asas anatarajiwa kufanya ziara maalum katika Mkoa huo, ambapo pia atakutana na Halmashauri Kuu za CCM Wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Katibu Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa wa Iringa imebainisha kuwa ziara hiyo inatarajia kuanzia Mufindi siku ya Jumamosi, Agosti 3, mwaka huu.

“Tarehe 3 Agosti 2024, Mufindi, Tarehe 4, Agosti, Kilolo. Tarehe 7 Agosti, Iringa Vijijini na mwisho atahitimisha tarehe 9 Agosti, Iringa mjini.

MNEC ASAS ameendelea kukiimarisha Chama katika Mkoa wa Iringa huku akiwa nguzo kwenye kushiriki miradi ya kimaendeleo kimkoa, Nyanda za Juu Kusini pamoja na Taifa kwa ujumla.

Pia, MNEC ASAS anasifika kwa Utendajikazi, Upole, Ustamilivu, Subra, Busara, Huruma na Mapenzi yake kwa Chama na Taifa lake vimeendelea kumjengea taswira njema ya Chama kwa Wananchi wote.

Aidha, amekuwa mstari wa mbele kwa kujitolea katika sekta za Afya, Elimu, Miundombinu, Mitaji ya Wafanyabiashara wadogo (Machinga), Vijana na Kinamama, Lishe Mashuleni, Michezo na mengine mengi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here