Mlawa: Jumuiya imara lazima iwe na chanzo chake cha mapato

0

Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya Bagamoyo, Aboubakary Mlawa amezielekeza Jumuiya za wazazi Kata kuanzisha mradi wa kiuchumi ili kuweza kujitegemea.

Akikagua mradi wa kilimo cha Muhogo wa Jumuiya ya Wazazi Kata ya Msoga alieleza, Kata hiyo ni mfano wa kuigwa na utekelezaji wa maagizo yake.

Alisema, Jumuiya imara lazima iwe na chanzo chake cha mapato halali ili kujiimarisha kiuchumi.

Mlawa alisema, mradi huo utakuwa chachu kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo katika kilimo hicho na ukizingatia uwepo wa soko la uhakika.

Aliongeza kuwa, yeye na Kamati yake ya utekelezaji itahakikisha kila Kata inakuwa na mradi na Wataongeza nguvu zao katika miradi mbalimbali ili adhma itimie.

Katika ukaguzi huo kamati hiyo iliweza kuchangia Shilingi 450,000 (Laki nne na nusu) na ahadi ya kugharamia ulimaji wa trekta utakaogharamiwa na Diwani wa Kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri Mwinyikondo.

Kamati hiyo pia inatarajia kuanza ziara hivi karibuni kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo, kuelezea utekelezaji wa ilani unaofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita sanjali na kusikiliza kero za wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here