Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeviasa Vyama vya Upinzani na kuvitaka vielewe maana ya demokrasia ya Vyama Vingi si kuizuia Serikali isitimize wajibu wake au ihofie kuchukua hatua za Kisheria pale itakapobidi.
Kadhalika CCM kimeutaja ushindani wa Kisiasa ikitaka uwe ni mchuano wa hoja na sera, si kukithiri matusi au kupandikiza hasama na chuki.
Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis Visiwani humu.
Mbeto yuko katika Msafara wa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ziara inayoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Akizungumza kwa masikitiko alisema inashangaza kwa baadhi ya Viongozi wa upinzani, wakisikika katika hotuba zao zikihamasisha hasama kwa lengo la kulipasua au kuligawa Taifa.
“Ushindani wa Siasa za chuki, hasama na matusi si kielelezo cha ustaarabu wa kisiasa. Tunawaonya wenzetu waache Siasa zisizo na manufaa kwao , kwetu na kwa jamii yetu,” alisema Mbeto.
Pia, Katibu Mwenezi huyo alisema tabia ya baadhi ya Wanasiasa kutoa vitisho au madai yasio na ushahidi, hakuthibitishi kupevuka kwao badala yake wananchi huwapuuza.
“Huwezi kubagaza Utu na heshima ya wenzako kisha uachwe ukitamba Mitaani. Vyombo vya dola na vya Kisheria vipo makini. Kutuhumu wenzako kwa masuala yasio na ushahidi si uungwana “Alieleza
Mbeto alisema, Siasa ni ushindani wa kimantiki unaoshindanisha hoja na sera. Tunaelewa kazi ya upinzani ni kufichua uovu ndani ya utawala lakini kuwe na ushahidi na vielelezo si kutamka matusi mbele ya jamii.
“CCM haijawahi kuhofia upinzani toka mwaka 1992. Walikuwepo kina Mabere Marando, Chifu Fundikira, Mapalala, Maalim Seif, Kambona na Mloo walikuwa hawakutoa matusi. Walitoa hoja na kujibiwa kwa nguvu ya hoja,” alifahamisha.
Aliwataja Viongozi hao huku akisifu kuwa walikuwa wamekomaa na wajenzi wa hoja makini na waliojua umuhimu wa Amani na Umoja bila kutoa vitisho au kueneza chuki za kisiasa.akizungumzia kauli ya makamu mwenyekiti wa ccm na Rais wa zanzibar kuhusu serekali ya umoja wa kitaifa na mazungumzo ya kusaka muwafaka,
Mbeto alisema, kauli ya Makamu Mwenyekiti na Rais Wazanzibar ipo wazi na ndio msimamo wa .
Aliongeza: “tutazungumza kwa yale mambo yanayo husiana na sheria ya serikali ya umoja wa Kitaifa kama kutakuwa na mambo ambayo hayapo kwenye yale mambo yaliyowekwa kwenye sheria,”
“Hayo yatahitaji maamuzi ya vyombo husika kama baraza la wawakilishi na vyombo vyengine vinavyo husika vilivyo wekwa na Katiba ya Zanzibar na sheria zake, huwezi kutaka mambo ambayo kwa mujibu wa Katiba yapo kwenye Mamlaka ya Rais.”