Mazungumzo ya Rais Samia na Appolo yazaa matunda

0

Na WAF – Dar es Salaam

UONGOZI wa Kituo cha Umahiri na Ubobezi wa Kimatibabu ‘Apollo Hospitali’ kilichopo nchini India umeanza kutathmini eneo itakapojenga Hospitali jijini Dar es Salaam ambapo uwekezaji huo utakaoleta chachu katika Sekta ya Afya.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu wakati wa mazungumzo na Rais wa Apollo Group Hospitals, Dkt. K. Hari Prasad kilichofanyika Jijini Dar es Salaam.

Alisema, mesema, majadiliano hayo yamefuatia kati ya Rais Samia na uongozi wa Hospitali hiyo yaliyofanyika Oktoba 11 mwaka huu ambapo hadi Sasa ni siku 27 tu zimepita tangu majadiliano hayo yafanyike.

Aidha, Dkt. Jingu alisema ndani ya miaka mitatu Hospitali hii itakuwa imeshajengwa na inafanya kazi, tuna kila sababu ya kumshukukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona jambo hili ni muhimu ambapo uwekezaji huo utazidi kuboresha huduma za Afya.

Wakati akiendelea kuelezea umuhimu wa Hospitali hiyo Dkt. Jingu alisema, hatua hiyo ni katika kuhakikisha Tanzania inakua na kituo cha umahiri ukanda wa Kusini mwa Afrika pia ukanda wa Afrika Mashariki.

“Tanzania imewekeza katika kuboresha huduma za Afya hivyo kituo hiko cha umahiri kitaongeza utalii wa matibabu na watu wote watakuja kupata huduma za Afya nchini,” alisema Dkt. Jingu

Kwa upande wake Rais wa Apollo Group Hospitals, Dkt. K. Hari Prasad wakati akizungumzia mchakato unaoendelea baada ya kikao cha siku tatu kati ya hospitali hiyo na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya amesema wamekuja Tanzania kuanzisha kituo cha matibabu bobezi ili kuongeza ubora wa huduma za Afya nchini.

“Sisi tunaziba pengo lililopo na hatuji kwa sababu ya mashindano na watoa huduma wengine, tunaamini katika hili na ujio wa bima ya afya kwa wote pia utasaidia watu kupata huduma bora zaidi Tanzania na Baraza la Afrika”. alisema Dkt. Prasad.

Alisema, katika mazungumzo yao na Rais Dkt. Samia ambapo amesisitiza namna watakavyosaidia kuleta huduma za kibingwa nchini ikiwemo matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo na hasa yale magonjwa ambayo bado Watanzania wanafuata huduma hizo nchini India.

“Tulisaini makubaliano kati ya Tanzania na India, tumekaa hapa kwa siku tatu, tumeangalia sera zilizopo na kuona eneo ambalo tutawekeza tumefurahi sana na tunaamini miaka miwili ijayo tutaweza kuanzisha huduma kwani tunashauku na hatuna wasiwasi kuwekeza Tanzania”. alisema Dkt. Prasad.

Nae, Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Tumaini Nagu alisema, wamekaa na uongozi wa Apollo kwa siku tatu na kufanya makubaliano kadhaa ikiwemo eneo ambalo Hospitali hiyo itajengwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here