WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema misingi ya Nchi ya Tanzania imetokana na Muungano ambao kila mmoja anapaswa kuulinda kwa nguvu zote.
Masauni amesema, Muungano wa Tanzania umekuwa mfano wa Mataifa mengi ambayo yameshindwa kuuendeleza Muungano wao, lakini misingi imara iliyowekwa na waasisi wa Taifa letu ndio uliosababisha uzidi kudumu.
Waziri Masauni ameyasema hayo Agosti 30, 2026 Unguja, Zanzibar aliposhiriki Ibada ya changizo ya Ujenzi katika Kanisa Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Augustino Kiboje, akieleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Kanisa katika kulea vijana katika maadili mema.
“Nchi yetu imejengwa katika Amani, upendo na Umoja ndio maana leo hii tumekutana hapa bila kujali mtu kabila lake wala dini yake kwa kuwa shule na hospitali nyingi zinazojengwa na makanisa zinahudumia watu wote bila kubagua.
“Siamini kama kuna Mtanzania ipo siku atachezea misingi hii iliyowekwa na waasisi wetu kwa kuangalia mifano ya mataifa mengine inavyoishi, nawasihi vijna tusichezea misingi iliyowekwa na waasisi wetu,” amesema Masauni.
kuwa wajibu wa kulinda amani ya Tanzania ni kwa kila mtu, hivyo suala la Muungano sio la kulitanzama kama jambo la kawaida.
Aidha, Masauni ameupongeza uongozi wa Kanisa Katoliki kwa namna ambavyo wamekuwa mstari wa mbele katika kusaidia malezi kwa vijana kupitia program mbalimbali zinazoanzishwa na kanisa hilo.