Na Sixmund Begashe, Dodoma
TIMU ya Maliasili Sports Club ya mpira wa Pete, ikiwa ipo kwenye maandalizi ya Michuano ya SHIMIWI 2026, imezichangamsha timu ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Ardhi kwa kuzifunga magoli 9-6.
Katika michezo hiyo ya kirafiki kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Uwanja wa Ndege, Dodoma, Maliasili ilianza kugawa dozi hiyo kwa timu ya TAMISEMI kwa mabao 9-6 na kwenye mchezo wa pili wa kutoana jasho na timu ya Ardhi, Maliasi ikaibuka tena na ushindi wa 9-6.
Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kuzinoa timu zake tayari kwa Michuoano ya SHIMIWI inayotarajiwa kuanza hivi karibuni Mkoani Kilimanjaro.