Mageuzi makubwa Wakala wa Vipimo

0

Na Albert Kawogo

SERIKALI kupitia Wakala wa vipimo nchini (WMA) imefanya mageuzi makubwa yanayolenga kumlinda mlaji kwenye huduma na ubora wa vipimo vinavyotumika katika sekta za biashara, afya na mazingira.

Mtendaji Mkuu wa WMA Alban Kiula alisema hayo Jijini Dar es Salaam wakati akiongea na Wahariri kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) ukiwa ni mfululizo wa vikao vya Taasisi za Umma zilizoko chini ya Msajili wa Hazina.

Kiula alisema, WMA ina jukumu kubwa la kuilinda jamii kwenye athari zinazotokana na matokeo ya upimaji usio sahihi katika biashara na maeneo mengine mtambuka. “Unaweza usiione hii hali, lakini kuna madhara makubwa kijamii yatokanayo na upimaji usio sahihi hasa kiuchumi.”

Mtendaji Mkuu alisema, jukumu la WMA haliishii kwenye kusimamia na kudhibiti vipimo, bali wanatoa ushauri wa kitaalam kuhusiana na vipimo kwa Serikali, mashirika ya umma na Taasisi binafsi.

Pia, Kihula alisema moja ya mafanikio makubwa ya WMA ni kuongezeka kwa idadi ya vipimo vinavyohakikiwa na kuendelea na ununuzi wa vifaa vya kitaalam ambapo yote haya yameipa thamani taasisi hiyo

Akizungumza kwa niaba ya Wahariri Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEF Deodatus Balile alisema, kazi kubwa ya kupongezwa imefanywa na WMA, lakini bado changamoto iko kwenye uchache wa watendaji kwa kuwa jukumu la WMA lina wigo mpana wa kiutendaji hasa kwenye yale maeneo yanayogusa walaji kwa bidhaa za chakula na vifaa vya ujenzi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here