Kitabu cha malezi ya watoto zama za Kidijitali chazinduliwa

0

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha ambaye ndiye mwandishi wa kitabu cha Elimu na malezi Kwa Watoto katika Zama Za Kidijitali amezindua kitabu hicho katika kijiji cha Kitangari Sokoni kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara.

Uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika hivi karibuni Dkt. Mnasi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotoa fedha nyingi za kutekekeza miradi nchini.

Pia, aliongeza kuwa licha ya kuwa na majukumu mengi ya kiserikali ila aliwiwa kuandika kitabu hicho cha Elimu na Malezi Kwa Watoto katika zama za kidigitali kutokana na Kasi kubwa ya ukuaji wa utandawazi.

Alisema, ukuaji huo kwa kiwango kikubwa unaathiri Mila na tamaduni kwa Jamii yetu hivyo kitabu hicho kinaenda kuwa suluhisho katikati Zama hizi Za utandawazi na ukuwaji wa technologijia.

Amewataka wazazi, walezi pamoja na Jamii kupata Nakala Za kitabu hicho ili kuwasaidia watoto katika namna Bora ya kujifunza na kupata Elimu pamoja na Malezi yaliyo bora ili kukuza Taifa lenye maadili mema na uchapakazi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here