Katibu Mkuu Wizara ya Madini ang’ara Afrika Kusini

0

KATIBU Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya ushauri ya Utawala na Sera katika Mkutano Mkubwa wa Madini na Uwekezaji Barani Afrika Maarufu kama Mining Indaba unaofanyika kila mwaka Cape Town, Afrika Kusini.

Mwezi Februari, 2024 mkutano huo ulitimiza miaka 30 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 ambapo k wa mara ya kwanza Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Madini ilishiriki kwa Pamoja kwa kushirikiana na Sekta binafsi kupitia Chemba ya Migodi Tanzania.

Kupitia mtandao wake wa kijamii wa X Katibu Mkuu Mahimbali alisema “nimefurahi kuheshimishwa kwa kuteuliwa kuwa Mjumbe wa Kamati ya Ushauri ya Utawala na Sera katika Mkutano wa Madini na Uwekezaji Afrika (Mining Indaba). Natarajia kuchangia katika mijadala na maamuzi muhimu kwa ajili ya Sekta ya Madini Afrika,’’.

Kufuatia uteuzi huo, viongozi na watumishi wa Wizara ya madini pamoja na wadau mbalimbali wamempongeza Katibu Mkuu Mahimbali ambapo Kamishna Msaidizi wa Madini sehemu ya Mazingira Wizara ya Madini Mhandisi Ally Samaje ameuelezea uteuzi huo kama heshima kwa Tanzania.

“Kimsingi Katibu Mkuu umekuwa mstari wa mbele kuipa heshima Sekta ya Madini na hii inathibitishwa na mialiko mingi kutoka pande za dunia kuona Tanzania ni nchi sahihi ya kuzungumzia masuala mbalimbali ya madini, tunajivunia wewe,’’ alisema.

Naye, Mkurugenzi Sera na Mipango Wizara ya Madini Augustine Olal ameuelezea uteuzi huo unaonesha ni kwa namna gani unaonesha Mahimbali amekuwa na mchango kwenye Sekta ya madini Tanzania.

Wakati Tanzania iliposhiriki mkutano wa Mining Indaba mwezi Februari mwaka huu, ilipata nafasi ya kushiriki kwenye majukwaaa mbalimbali kutoa uzoefu wake katika shughuli za madini ikiwemo kukutana na wadau mbalimbali walioonesha nia kuwekeza kwenye sekta ya madini nchini kupitia mikutano ya ana kwa ana.

Aidha, katika mkutano huo Tanzania ilijikita katika kuendelea kuzinadi fursa zake za kiuwekezaji kwenye mnyororo mzima wa shughuli za madini ikihusisha shughuli za utafiti, uchimbaji madini, uongezaji thamani madini, usambazaji wa vifaa na utoaji huduma migodini.

Mkutano wa Mining Indaba huwakutanisha wadau mbalimbali wa madini kutoka maeneo mbalimbali duniani zikwemo Serikali, kampuni kubwa cha uchimbaji, watendaji wakuu wa kampuni kubwa za madini duniani, watoa huduma, wauzaji wa bidhaa za madini, taasisi za fedha na wadau wengine muhimu kwenye sekta hiyo.

Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo uliongozwa na Naibu Waziri Dkt. Steven Kiruswa akiambatana na Katibu Mkuu Kheri Mahimbali, Naibu Katibu Mkuu Msafiri Mbibo viongozi wengine wa Wizara na Serikali pamoja na wadau wengine wa Sekta ya Madini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here