-
Na Maalum Mwandishi
TANGU mwanzo wa vita vya Israeli dhidi ya Gaza, Misri haijaacha juhudi zozote za kuwasaidia watu wa Palestina, ikiongeza usaidizi wake usio na kikomo kwa Wapalestina katika ngazi zote (kisiasa, kibinadamu, kiulinzi, kiusalama na kiutu).
Juhudi za Kisiasa:
Katika juhudi zake za Kisiasa kurejesha Amani na utulivu kwenye ukanda wa mashariki ya kati, Misri imejitahidi kadri ya uwezo wake kufanya yafuatayo;
Mosi, Misri imefanya juhudi za mawasiliano na pande mbalimbali husika na mgogoro huo, na kuzaa mikutano ya pande zote ikijumuisha wanahabari.
Uongozi wa kisiasa wa Misri umerudia kukataa kwake kabisa mipango ya kuwasukuma Wapalestina kuhama kwa hiari au kwa nguvu kutoka katika ardhi yao na kutafuta suluhu mbadala inayoakisi Amani ya kudumu na Israel.
Pili, imefanya mkutano wa kwanza wa Kimataifa kuhusu maendeleo ya kusaka Amani ya kudumu Gaza na Mashariki ya kati kwa ujumla (Mkutano wa Amani wa Cairo) mnamo tarehe 21 Oktoba 2023, na michango mipana ya kimataifa.
Kumekuwa na mwitikio chanya kutoka kwa baadhi ya nchi zinazoshiriki, hivyo kutuma ujumbe wazi kwa ulimwengu kuhusu msimamo thabiti wa Wamisri kuelekea mgogoro huo.
Tatu, Misri imefanya mkutano wa kilele wa Waarabu na Waislamu huko Cairo mnamo Machi 2025, ambapo makubaliano yalifikiwa kuhusu mpango wa Misri wa ujenzi upya wa Gaza.
Nne, Misri imetoa hoja mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki, kubainisha desturi za Israeli katika maeneo ya Palestina, huku ikidokeza nia ya Cairo kujiunga na kesi iliyowasilishwa na Afrika Kusini dhidi ya Israeli katika Mahakama hiyo.
Tano, Misri imedumisha mawasiliano na pande zote za kikanda na kimataifa tangu mwanzo wa mgogoro, ili kuhamasisha jumuiya ya kimataifa kuunga mkono maono ya Misri katika suala hilo (kukataa uhamisho wowote wa Wapalestina, na kuinasihi Israeli kuchukua jukumu lake kama taifa kuunga mkono Mamlaka ya Palestina kuanza tena utawala wa Ukanda wa Gaza baada ya vita).
Sita, Misri imeimarisha Juhudi za kuunganisha safu za Wapalestina mbele kuzuia kuwondoa kwenye maeneo yao kama ilivyopendekezwa na Israel.
Katika suala hilo, Misri iliandaa mikutano na vyama vya HAMAS pamoja na FATAH mnamo Oktoba 2024, ili kuunga mkono maridhiano ya kitaifa, na kufanya mipango inayohitajika kwa “Siku za Baadaye” (baada ya kupatikana Amani).
Pande hizo mbili zilipitia na kujadili pendekezo la Misri la kuanzisha kamati ya usaidizi wa jamii kusimamia Ukanda wa Gaza.
Saba, ili kuthibitisha hitaji la juhudi za baada ya vita na kuwezesha kuanza tena kwa mchakato wa kisiasa kati ya Wapalestina na Waisraeli, Misri ikaandaa Mazingira yanayofaa kulingana na hatua sahihi kupata suluhisho la Mataifa mawili; ikiwa ndiyo njia pekee ya utulivu katika Mashariki ya Kati.
Ikumbukwe kwamba, suluhu yoyote iliyofungwa kwa hadhi ya baadaye ya Gaza, haitasababisha uwepo wa amani ya kudumu, kutokana na ukweli kwamba Wapalestina wamepoteza matumaini ya suluhu ya kisiasa kwa suala lao.
Mazungumzo ya Kusitisha Vita kati ya Israeli na Hamas:
Misri imefanya jitihada kubwa kusimamisha vita wa sababu za kibinaadamu wa siku Saba mnamo Novemba 2023, kutokana na mawasiliano yake na upande wa Israeli, pamoja na vikundi vya Wapalestina kupitia uratibu na Qatar na Marekani.
Makubaliano hayo ya awali ya kusitisha vita yameshuhudia kuachiliwa kwa Mateka Waisraeli 80, miili Mitatu na watu 22 kutoka mataifa mengine.
Kwa upande mwingine, Israeli iliwaachilia huru Wapalestina 240 wanawake na watoto kutoka magerezani, huku ikipanua ufikiaji wa raia wa Gaza kwa misaada ya kibinadamu.
Juhudi za Misri zikaimarishwa zaidi kwa uratibu Qatar na Marekani, kufikia makubaliano ya pili ya kusitisha mapigano mnamo tarehe 19 Januari 2025.
Mkataba huo uligawanywa katika awamu tatu za siku 42, ambapo mateka 33 wa Israeli waliachiliwa huru, badala ya kuwaachilia wafungwa 1924 wa Kipalestina.
Katika kipindi hicho malori 600 ya misaada yaliruhusiwa kuingia Gaza kila siku, Israeli iliondoka polepole kutoka baadhi ya maeneo huko Gaza, na kivuko cha mpaka cha Rafah kilifunguliwa tena ili kuruhusu Wapalestina 50 waliojeruhiwa kuondoka kila siku kupata matibabu zaidi nje ya nchi.
Hata hivyo, upande wa Israeli ulizuia awamu zingine za makubaliano, kupitia operesheni yake ya kijeshi ya upande mmoja, dhidi ya Ukanda wa Gaza mnamo tarehe 18 Machi 2025, na kusababisha mapigano kuanza tena.
Mnamo Aprili 2025, Qatar na Marekani zilifanikiwa kuishawishi HAMAS kumwachilia mateka wa Israeli wa Marekani, Alexander Edan, bila masharti kama ishara ya nia njema ya kuthibitisha kwamba, inatafuta kwa dhati kusitisha mapigano huko Gaza na kujibu juhudi za wasuluhishi.
Mnamo tarehe 15 Agosti 2025, Wasuluhishi waliwasilisha pendekezo ikiwa ni pamoja na makubaliano ya muda ya kusitisha mapigano (siku 60 za kusitisha mapigano), kuwaachilia mateka 10 na miili 18, pamoja na kuruhusu usambazaji wa misaada kulingana na utaratibu wa makubaliano ya tarehe 19/1/2025.
Pia, kuanzisha mazungumzo tangu siku ya kwanza kati ya pande hizo mbili, kuhusu mipango inayohitajika ya Wasuluhishi wa kudumu na Marekani, ya kuhakikisha uendelevu wa kusitisha mapigano ndani ya siku 60.
Wakati huo Rais Trump wa Marekani akaihakikishia Misri juu ya kuwepo mwendelezo wa mazungumzo mazito kwa muda wa ziada, ili kupata suluhu kwa ukamilifu wake, ambapo HAMAS ilishajiishwa na kukubali. Hata hivyo, kwa masharti magumu yaliyowekwa na Israeli, pendekezo hilo lilizuiwa.
Misri pia imechangia kuendeleza juhudi za kuanza tena mazungumzo baada ya mgomo wa Israeli dhidi ya ujumbe wa HAMAS huko Doha mnamo tarehe 09 Septemba 2025.
Juhudi za Kibinadamu na za Kijamii:
Juhudi za Serikali ya Misri za kupunguza athari za mgogoro wa kibinadamu huko Gaza hivi karibuni, zimezaa matunda.
Kupitia kuratibu kwa pamoja na mashirika ya kimataifa ya misaada, Misri imewezesha mtiririko wa misaada inayohitajika, ambayo inapokelewa katika uwanja wa ndege wa Al-Arish huko Sinai Kaskazini (Misri hutoa takriban asilimia 80 ya misaada ya kibinadamu).
Pia, Serikali ya Misri imesaidia kuimarisha mawasiliano na upande wa Israeli tangu tarehe 08 Mei 2024, baada ya kuchukua udhibiti wa kivuko cha Rafah kutoka upande wa Palestina, na kuimarisha uwepo wake katika ukanda wa Philadelphia.
Msimamo wa Misri katika suala hilo ulikusudiwa kuongeza shinikizo, la kuongeza mzunguko wa utoaji wa misaada katika ukanda, kupitia kivuko cha Kerm Abu Salem, huku ikitaka kufungua vivuko vyote na Gaza, hivyo kuongeza idadi ya malori yanayoingia kila siku (malori 250 kila siku hivi sasa).
Hitimisho:-
Ikumbukwe kuwa, mnamo tarehe 02 Desemba 2024, Misri iliandaa mkutano wa kibinadamu kuhusu hali ya Gaza ili kutoa msaada unaohitajika, ili kuzuia kuzorota zaidi kwa hali hiyo, pamoja na kujadili mipango inayohitajika ya kuanza ujenzi upya wa Gaza.
Misri pia imewezesha kuanzisha kambi za Wamisri kwa ajili ya Wapalestina waliokimbia makazi yao ndani ya Gaza (huko Deir el Balah-Rfah-khan Younis), ili kuwapa msaada na huduma.
Zaidi ya hayo, Misri imesaidia kuishajiisha Israeli kufungua tena vivuko vya Gaza, na kuondoa vikwazo vyovyote vinavyozuia utoaji wa misaada ya kila siku.