MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Serikali ina mpango wa kufanya uwekezaji mkubwa katika eneo la Hoteli ya Bwawani katika awamu ijayo ya uongozi wake.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni Jimbo la Malindi, Mkoa wa Mjini Magharibi, leo Septemba 29, 2025, Dkt. Mwinyi alibainisha kuwa eneo hilo ni muhimu kwa uchumi na utalii wa Zanzibar, na Serikali inalenga kulibadilisha kuwa mfano bora wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aidha, ameeleza kuwa Serikali ya awamu ijayo pia itatekeleza mpango maalum wa kuimarisha nyumba zote za Mji Mkongwe zikiwemo nyumba za wakfu, binafsi na za Serikali ili ziendelee kudumu kwa muda mrefu, kwa kutumia fedha za ndani.
Kuhusu changamoto ya magari kuingia Mji Mkongwe, amesema Serikali imekamilisha mpango wa mabasi ya umeme ili kupunguza tatizo hilo na kulinda uimara wa majengo ya kihistoria.
Halikadhalika, Dkt.Mwinyi amewahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali itatenga maeneo rasmi ya biashara ili kuwaondolea usumbufu wa kuhamishwa mara kwa mara.
Rais Mwinyi aliwatembelea vijana wa Makachu Forodhani, Bustani ya Afrika House iliyowekezwa upya, pamoja na Klabu ya Muziki wa Taarabu la Culture lililofanyiwa ukarabati mkubwa, na kuwasisitiza kuendeleza vipaji vya muziki wa taarabu.
Amewaomba wananchi wa Jimbo la Malindi na Wazanzibari kwa ujumla kumpa tena ridhaa ya uongozi ili aendelee kutekeleza kwa ufanisi ahadi alizoahidi,