Rais Mwinyi: Uchaguzi Mkuu utafanyika kwa amani na utulivu

0

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewahakikishia Wananchi kuwa Uchaguzi Mkuu Ujao Utafanyika kwa Amani na Utulivu.

Alhaj Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipotoa Salamu baada ya Kujumuika kwa Sala ya Ijumaa Masjid Raudha Uliopo Darajabovu, Mkoa wa Mjini Magharibi Aprili 4, 2025.

Amefahamisha kuwa, dhamira ya Serikali anayoiongoza ni kuona Uchaguzi huo kuwa ni Kielelezo cha kuwepo kwa Amani ya kudumu hapa Nchini na kila Mwananchi anapata fursa ya kutekeleza haki ya Msingi ya Kikatiba ya kupiga Kura.

Rais Dkt. Mwinyi alisema ni Wajibu wa Msingi wa kila Mwananchi Kuhakikisha Amani iliopo inadumishwa wakati huu na Baada ya Uchaguzi Ili Nchi ipige hatua zaidi za Maendeleo katika Nyanja tofauti.

Aidha, amewanasihi Waumini wa Dini ya Kiislamu Kuendeleza utaratibu wa Kuwasaidia Watu wanaohitaji Misaada kama ilivyofanyika vema wakati wa Mwezi wa Ramadhani.

Halikadhalika Rais Dkt. Mwinyi ameeeleza kuwa Mwenendo Mzuri uliotekelezwa wakati wa Ramadhani unapaswa kuendelezwa kwa kiwango kile kile kwani bado makundi ya Wanaohitaji Kusaidiwa yapo ndani ya Jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here