‘Sera ya mamlaka kamili ya ACT inaandaa uasi na mapinduzi’

0

Mwandishi Wetu, Zanzibar

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar kimebainisha kuwa sera ya Chama cha ACT Wazalendo ya kutaka mamlaka kamili Zanzibar ni kuunda uasi na kufanya mapinduzi dhidi ya maendeleo yanayopatikana hivi sasa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis.

Mbeto alitoa kauli hiyo kufuatia matamshi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar ambaye pia ni Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman.

Akiwa katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kivunge, Kaskazini Unguja hivi karibuni, kiongozi huyo wa ACT Wazalendo alidai kuwa uchaguzi mkuu 2025 ni wa kuipatia Zanzibar mamlaka kamili.

Akijibu hoja hiyo Mbeto alisema, kauli ya kiongozi huyo ni kuwadanganya wanachama wa ACT Wazalendo, kwani kitendo hicho hakiwezekani ni sawa na kuandaa uasi unaorudisha nyuma maendeleo ya kiuchumi, kisiasa na kijamii yaliyopatikana ndani ya miaka 60 ya Muungano.
“Kitu hicho hakiwezekani.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here